Wednesday, April 16, 2014

Sina Mpango Wowote Wa Kumuoa Chuchu Hans: Ray

Ray na Chuchu Hans
Swali ambalo wengi watakuwa wakijiuliza kwasasa ni je Star wa filamu nchini Vicent Kigosi"Ray" anamchezea tu Chuchu Hans lakini hana mpango nae kimaisha !. Swali hilo pia linaweza kuibuka kichwani mwa Chuchu mwenyewe ambaye pia ni star aliyejijengea jina katika filamu Swahiliwood. Well, akizungumza na Globalpublishers Ray amesema kuwa hana mpango wa kuoana na Chuchu Hans hata kama akipewa talaka na aliyekuwa mumewe. "Sina mpango wa kuoa ndugu yangu, hayo ni maneno ya watu ambayo yapo tu mitaani ila kwa sasa niko njiani naenda gym baadaye nitakutafuta tuongee" alisema Ray ambaye filamu zake nyingi zinafanya vizuri sokoni.

Hata hivyo inawezekana Ray ameyasema hayo ili kuepuka kufuatwafutwa na mapaparazi katika penzi lake na Chuchu ambaye aliibuka Miss Talent katika Miss Tanzania 2005.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment