Friday, April 18, 2014

Ukaribu Wa Lulu Na John Mnyika Wazua Hofu Na Minong'ono.

Star wa filamu Swahiliwood mwenye umaarufu mkubwa tofauti na umri wake mdogo Elizabeth Michael "Lulu" amezua hofu kwa baadhi ya watu wanaofuatlia mambo na maisha ya mastaa kwa kudaiwa kuwa karibu sana na Mbunge wa Ubungo John Mnyika. Habari hizo za chinichini ambazo kwasasa zinadaiwa kusambaa kama moto wa kifuu ni kuwa ukaribu wa Lulu na Mnyika ambaye ni mmoja wa wanasiasa vijana wanaokubalika nchini sio bure lazima kuna jambo. Habari zaidi zinadai kuwa hivi juzi kati Lulu alitia team Dodoma na mwenyeji wake alikuwa Mh. Mnyika.
Hata hivyo star huyo aliyejaaliwa mvuto mkubwa unaowatoa udenda wanaume wengi alipotafutwa na Visa na kuulizwa juu ya madai hayo alikana kwa kusema "Hayo mambo ndiyo nayasikia kwako, hakuna kitu kama hicho na wala sijawahi kwenda Dodoma tangu nitoke matatizoni huo ni upuuzi tu wa maneno ya watu"

                                                                     John Mnyika akiwa Bungeni
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment