Wednesday, July 23, 2014

Rehema Nkalami Wa Swahili Talk Radio Denmark Avamiwa Na Majambazi Dar es salaam.

Rehema aliyevaa jeans akiwa na wageni wake walipotembelea watoto yatima
Mtangazaji wa Swahili Talk Radio ya nchini Denmark Rehema Amiry Nkalami ambaye ni mtanzania amevamiwa juzi na majambazi eneo la Morocco, jijini Dar es salaam.
Majambazi hao walimvamia Rehema akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka 15 pamoja na wageni wengine aliokuja nao kutoka Denmark wakati wakielekea katika kituo cha watoto yatima kuwaaga baada ya siku chache nyuma kutoa misaada mbalimbali ki. Akizungumza na SWP Rehema alisema kuwa majambazi hao walikuwa na silaha na waliwanyang'anya kila kitu walichokuwa nacho zikiwemp passport zao wote, pesa taslim Tsh. mil. 2.5, Ipad5 na vitu vingine.
walipotembelea watoto yatima
'tumevamiwa na majambazi wa bastora kwenye gali na wakatupora kila kitu hata dokment zangu za kusafiria . sasa nangoja Denmark watengeneze docment mpya, ndio nahangaika hivi, pia wameiba camera ,ipad5, 2,5 million sh.bank kadi zangu na za watoto zote, driving liecens, hearth insurance kadi zangu na za watoto, Passport zetu zote"

'walitumia kitako cha bunduki kuvunja kioo cha upande wangu, vipande pande vya chupa vikaingia upande wa pega ambalo lilielekea upande wa kile kioo, nilikua Burhani hospita kutolewa vioo hivyo, juu Burhani hospitol ndio hospitali ambayo tuna health insurance ya familia nzima tokea miaka zaidi ya ishillini wakati naishi hapa, namshukuru Dr Self kwa huduma nzuri.watoto wangu wa miaka 15 na mimi ndio tulikuwa kwenye gari hilo'

"polisi kutoka oystabay police walikuja kwenye tukio kisha wakatuchukua kituoni kwa ajili ya kutengeneza report., katika majadiliano na polisi waliamua kumuweka ndani driver wanadai ndio alietuuza kwa majambazi, tulikuwa tunaelekea kwenya kitua cha yatima kuwaaga watoto ambao wiki iliyopita tulipeleka msaada huko"


Mgeni wa Rehema alipotembelea watoto yatima 
Rehema alitaka kuondoa nchini kurudi Denmark jana lakini ilishindikana kutokana na tatizo hilo kwasababu majambazi hao walichukua nyaraka zao muhimu na pia passport zao wate ambapo wanafuatilia kwasasa ubalozini ili wapate mpya waondoke.

Tungependa kuwapa pole kwa masahibu hayo yaliyowapata.

No comments:

Post a Comment