Friday, August 29, 2014

Wema Sepetu Anakuja Na Kitu Kikubwa Cha Kufungia Mwaka: Martin Kadinda

Meneja wa Wema Sepetu , Martin Kadinda amesema kuwa Wema Sepetu anatarajia kufanya kitu kikubwa mwishoni mwa mwaka huu baada ya kuwa kimya kwa muda. Akizungumza na Bongo5 Martin alisema kuwa kwasasa hawezi kutaja ni kitu gani kwasababu bado kipo hatua za awali lakini watu wajue Wema anakuja na kitu kikubwa. Vilevile Kandinda alisema kuwa msimu mpya wa reality show ya Wema "In My Shoes" utaanza rasmi mwezi ujao September

"Kuna vitu vingi ambavyo Wema anavifanya so far show inarudi mwezi September 'In My Shoes" something big Wema anafanya mwisho wa mwaka huu" alisema Martin

Na kuongeza "Kweli Wema hajafanya vitu karibuni lakini watu wasubiri mambo makubwa, hajaamua tu kukiweka kwenye media, mpaka vitu vinavyotakiwa vikishawekwa sawa. Sometime huwezi kuongea jambo ambalo hata halijafikia asilimia 50 ya jambo. Endless Films ipo na kuna jambo ambalo kama kampuni Wema anatakiwa afunge nalo mwaka ambalo is something big, kwahiyo watu wasubirie wataona nini Wema amekifanya"

No comments:

Post a Comment