Friday, September 19, 2014

Diamond Ataka Wema Amzalie Mtoto, Wema Akataa Kuogopa Kupoteza Mvuto Na Umaarufu, Diamond Amrushia Dongo !

Wema na Diamond
latest star's buzz ni kuwa  Diamond Platnumz kwa muda sasa amekuwa akimwambia mpenzi wake Wema Sepetu abebe mimba kwasababu yeye anataka mtoto lakini Wema amekuwa mgumu kukubali kudungwa mimba na Diamond kwasasa kwa madai kuwa hayupo tayari kuzaa muda huu sababu ikiwa ni kuwa atapoteza mvuto wake kiumbo na pia kuchuja kiumaarufu, kitu ambacho hakitaki.
Chanzo kilicho karibu na Wema na Diamond kimeiambia Swahiliworldplanet. kwa kusema...
"ni muda sasa Diamond anataka mtoto tatizo ni bidada Wema hataki anaogopa kushuka umaarufu na pia kupoteza umbo lake lenye mvuto, kitendo hicho kimemuweka dilemma Diamond because pesa anayo ya kutosha kulea mtoto ila hailewi kwanini Wema hataki wapate mtoto now kwa kisingizio cha kupoteza fame yake na umbo" kilisema chanzo hicho kikiomba kutotajwa jina

Hata hivyo Diamond juzi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliweka post inayoshabihiana na maelezo ya chanzo hicho. Diamond ni kama alikuwa amerusha Dongo hilo kwa Wema kwa kuandika ...
"Kwa mtazamo wangu mimi naona kuzaa hakumfanyi mtu azeeke au awe wa kizamani, ni tabia tu ya mtu mwenyewe.... na ndio maana dada zetu kama Beyonce, Nancy sumary, Kim Kardashian na kadhalika wana watoto na still wanafanya vizuri.....Au we mtazamo wako ukoje?........ "

Vile vile mapema wiki hii gazeti moja la burudani liliandaka habari inayokaribiana maana na hii kuwa Wema hataki kuzaa kuogopa kupoteza mvuto wake na umaarufu"



Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment